*KESHA LA ASUBUHI*
*_30 MACHI 2019_*
*UZOEFU HAI NA WA KINA*
*_Sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Waebrania 2:3_*
✍🏾 Niliona ya kwamba hatupaswi kuahirisha suala la ujio wa Bwana. Malaika alisema: “Jiandaeni, jiandaeni, kwa ajili ya kile kinachokuja duniani. Hebu kazi zenu zipelekane na imani yenu. “Niliona ya kwamba mawazo yanapaswa kuwekwa kwa Mungu, na mvuto wetu unapaswa kumshuhudia Mungu na kweli yake.
✍🏾 Hatuwezi kumheshimu Bwana hali tukiwa wazembe na tusiojali. Tunapaswa kuwa makini katika kuthibitihsa wokovu wa roho zetu wenyewe, na pia kwa ajili ya kuwaokoa wengine.
✍🏾 Tunapaswa kulipatia jambo hili umuhimu wote, na mengine yote yatafuatia.
✍🏾 Niliona uzuri wa mbinguni. Nilisikia malaika wakiimba nyimbo za furaha, wakiimba sifa, heshima, na utukufu kwa Yesu. Kisha nikatambua kitu kuhusu upendo wa ajabu wa Mwana wa Mungu. Aliuacha utukufu wote, heshima yote aliyokuwa nayo mbinguni, na alipendezwa sana na wokovu wetu kiasi cha kuwa mnyenyekevu katika kujitwika kwa uvumilivu kila namna ya ufidhuli na dharau ambayo mwanadamu alimtupia.
✍🏾 Alijeruhiwa, akapigwa, na kuumizwa; alitundikwa katika msalaba wa Kalvari na kufa kwa maumivu makali zaidi ili kutuokoa na mauti, ili tupate kuoshwa katika damu yake na tufufuliwe kuishi pamoja naye katika makao anayotuandalia, ili tufurahie nuru na utukufu wa mbinguni, kusikia malaika wanapoimba, na hata kuimba pamoja nao.
✍🏾 Niliona ya kuwa mbingu yote inapendezwa na wokovu wetu; na je, sisi tusijali? Je, sisi tutuakuwa wazembe, kana kwamba suala la wokovu wetu ni jambo dogo? Je, tutadharau kafara ambayo imetolewa kwa ajili yetu?
✍🏾 Tumepewa kitabu ili kiongoze miguu yetu inapopita katika hatari za ulimwengu huu wenye giza na kuingia mbinguni. Kinatuambia jinsi tuwezavyo kuepuka ghadhabu yaMungu, na pia kinatuambia juu ya mateso ya Kristo kwa ajili yetu, kafara iliyo kuu ambayo imetolewa ili tupate kuokolewa na kufurahia uwepo wa Mungu milele.
✍🏾 Mfano wa utauwa hautamwokoa yeyote. Wote wanapaswa kuwa na uzoefu wa ndani kabisa na ulio hai. Hii ndiyo njia pekee ya kuwaokoa wakati wa taabu. Kisha kazi zao zitapimwa kwa jinsi zilivyo; na kama zipo kama dhahabu, fedha, au vito vya thamani zitafichwa sirini mwa hema la Bwana.
*BARIKIWA NA UWE NA IBADA NJEMA*


No comments: